Kwa sasa unapozungumzia ngoma ya kibao kata ambayo asili yake ni mkoani tanga, basi ni lazima utamtaja kijana anaesumbua vichwa vya watu wazima kwa masongi yake ambae ni kivurande junior.
Kijana huyu ambae pia ni mwenyeji wa mkoa wa tanga alianza kuimba taarab akiwa kwao tanga mjini, alipoona amepevuka kiasi alipanda basi na kuja dar es salaam kutafuta maisha na kuendeleza fani yake zaidi, bendi yake ya kwanza kuimbia hapa dar ni king's modern taarab iliyokuwa ikiongozwa na hamisi majaliwa sambamba nae director kijoka. pale kijana huyu alifanikiwa kurekodi wimbo wake wa kwanza kabisa ambao ulikuwa unakwenda kwa jina la "mtoto dot.com".
Baadae aliihama bendi hiyo na kujiunga na bendi ya t motto modern taarab chini yake mkurugenzi Amin salmin, pale alikutana na wasanii nguli kama jokha kassim, nyawana fundikila, aisha masanja, nassor hussein "chollo" thania msomali, shinuna kassim na wengineo wengi, lakini safari hii hakufanikiwa kurekodi akiwa na t motto modern taarab, bendi illipoanza kuyumba alijisogeza east african melody ambapo alifanya sana mazoezi na bendi hiyo na kushiriki show mbalimbali za bendi.
Kutokana na uimbaji wake mzuri, siku moja iliandaliwa show ya pamoja kati ya kibao kata na east african melody, aliponyanyuka kivurande kuimba ndipo viongozi wa kibao kata wakamuona na kuanza taratibu za kumnyakuwa moja kwa moja!, na kweli walifanikiwa kumchukuwa na sasa yeye ndio reader pale mbele katika uimbaji, unapomkuta stejini akifanya yake ndani ya billicanas club kila siku ya jumatano unaweza kumtunza pesa zote za mfukoni kwako ukakosa hata nauli ya kurudia nyumbani, wadau na wapenzi wake kwa sasa wamempachika jina wanamuita "mfalme wa kibao kata" jina ambalo kivurande amesema kuwa amelipokea kwa maana sio baya na mashabiki wake ndio wanaomkubali kwa kazi zake nzuri, mpenzi msomaji wa blog hii bora unaombwa kwenda pale billicanas club kila jumatano umuone kijana huyu anavyoisimamisha dar kwa kipaji chake alichojaaliwa na mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni