TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 31 Mei 2016

PRINCE AMIGO:- MKE WANGU HABIBA SI MKOROFI KAMA INAVYOSEMEKANA MIDOMONI MWA WATU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


PRINCE AMIGO AKIWAJIBIKA STEJI SAMBAMBA NA WACHEZA SHOW WA JAHAZI.

         Kwanza kabisa napenda niwaombe radhi wapenzi wasomaji wa blog hii bora ya ubuyu wa taarab kwa kuchelewa kuwaletea kikaango hiki kilichokuwa kikimuhusu prince amigo wa jahazi modern taarab na hii ni kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu ila leo nawaletea mfululizo huu wa maswali na majibu kama ifuatavyo:- 


 SALMA WA MAISHA FM DODOMA:- Amigo napenda kujua safari yako ya muziki wa taarab ulianza lini, na je ni nini siri ya mafanikio yako katika bendi ya jahazi modern taraab maana una muda mrefu licha baadhi ya wasanii kuhamahama bendi.


PRINCE AMIGO:- Safari yangu ya muziki wa taarab ilianza mwaka 2007 na kuhusu mafanikio niliyoyapata sihaba mpaka sasa najenga na pia nina usafiri wangu binafsi na maisha yangu mazuri tu namshukuru mwenyezimungu.


HOTIE GENERATION FM MBEYA:- Wewe kama msanii wa taarab unazungumziaje suala la wasanii kudharau wito wa watangazaji wa mikoani katika kufanya interview?.


 PRINCE AMIGO:- Ahsante sana bibie hotie, kwa mimi binafsi sina hiyo tabia pale ninapohitajika huwa nafika kwa wakati, na mimi namilikiwa kwahiyo naamlishwa tu na viongozi, kuhusu wasanii wengine kiukweli sijui, labda wengine wanafika huko mikoani wamechoka wanahitaji walale kidogo ili usiku waingie katika show nahisi hiyo ndio sababu ila kama wanakuwa na sababu tofauti mimi sijui.


NADYA BOMBA FM ZNZ:- Skendo zinasaidia kumpushi msanii kijina, kwa upande wako wewe skendo unazikubali kama ndio ni kwanini na kama hapana ni kwanini?.


 PRINCE AMIGO:- Aaah! kwangu mimi skendo sina, na kwanza haziwezi kunisaidia chochote sana sana zitaniharibia tu kwasababu kwanza ni kijana ambae natafuta maisha kwa njia kubwa ya kufika mbali alafu leo hii skendo za kijinga sio nzuri, kwangu mimi skendo haziwezi kunisaidia maana hazina faida, mimi kwangu kazi tu ndio ambayo inanisaidia.


 MC CHINGA DODOMA FM:- Inasemekana umetengana na mke wako mkubwa mama man je ni kweli? na pia kuna tetesi kuwa unampenda sana mke mdogo sababu ana pesa na kichokufanya umrudie mke mdogo ni nini?.


  PRINCE AMIGO:- Aaah! ni kweli nimemuacha mke mkubwa na sijarudiana na mke mdogo eti sababu ana pesa, mapenzi ni kupendana mioyoni na wala mapenzi sio pesa, kama ingekuwa ni pesa basi naamini nisingeweza kumuacha kwanza alafu nikamrudia, nilimuacha nikamfundisha na atambue kuwa mume wake nahitaji hiki na hiki na nilipomrudia ni sababu ya mapenzi na nyota yake na yangu zilikuwa zinaendana, na mku mkubwa nimemuacha kwasababu zangu mwenyewe binafsi na ni ngumu sana mtu mwingine kufahamu.


  SHUFAA KAYA FM BAGAMOYO:- Amigo, kuna tetesi kuwa mke mdogo ni mkorofi sana na amekuwa akimrusha roho mama man kila walipokuwa wakikutana, wewe kama mume ulikuwa unachukuwa hatua gani kwa tabia hii ya mke mdogo?.


 PRINCE AMIGO:- Bibie shufaa, kwa sasa nina mke mmoja tu anaitwa habiba ama zuu kama anavyofahamika mitandaoni, na hilo suala kwamba walikuwa wakikutana na kurushana roho ilikuwa kipindi hiko sana wakati nipo nao wote wawili lakini baada ya kumuacha mmoja na yule mwingine alitulia kwahiyo sikweli kwamba mke wangu huyu ni mkorofi au eti akikutana na mwenzie anamrusha roho hapana, wanawake mnajitambua jinsi mlivyo shufaa! kifupi mke wangu mdogo hana tatizo kabisa.


 FORTNA CG FM TABORA:- Prince amigo napenda kujua toka kwako mpaka sasa ni ndoa ngapi umeoa na umeacha ndoa ngapi na kwanini?.


 PRINCE AMIGO:- Mimi nilikuwa na ndoa mbili nimeacha ndoa moja na nimebaki na ndoa moja na ukiniuliza sababu ya kwanini hilo ni suala langu mimi mwenyewe binafsi ni vigumu kuliweka wazi.


 MWAJUMA RAS FM DODOMA:- Amigo una mikakati gani katika kujiendeleza kimuziki nje ya bendi yako ya jahazi modern taarab?.


  PRINCE AMIGO:- Suala la kujiendeleza kimuziki nje ya bendi yangu ya jahazi modern taarab, sijalipa nafasi ya kuliongelea sana ila naamini ni hivi karibuni tu wapenzi watafahamu mimi ni kitu gani ninachofanya, lakini kwa sasa nafuata kile ninachoambiwa kufanya ndani ya kampuni ya jahazi entertainment, mimi ni mwanamuziki ambae nina nidhamu kubwa sana wala sio mtu wa kukurupuka ovyo! ila nina plani kubwa sana ya kufanya kazi kubwa sana nje ya jahazi modern taarab lakini kwa sasa sijafikilia kufanya.


 AISHA WA BARMEDA'S TV MWANZA:- Mie nataka kujua kuna taarifa kwamba gari unayotembelea ni mali ya bi mdogo habiba, na kwake umefuata pesa sio mapenzi je swala hili ni kweli amigo?.


 PRINCE AMIGO:- Unajua siku zote anaejua siri ya mwenzie ni moyo wa mwenzie kwahiyo mara nyingi ukiruhusu kusikiliza sikio lako likasikia kila kitu basi mimi naamini unaweza kuja kusikia taarifa ukajakufa kwa presha katika kipindi unachotangaza bibie aisha, hayo yanayoongeleka yanaongeleka tu ila unatakiwa utambue kuwa mimi nafanya kitu gani katika maisha mimi ni mwanamuziki ambae ni mkubwa na najiamini kwenye hilo kwahiyo siwezi kusema mengine zaidi ila yoyote yanayoendelea katika maisha yangu ni maendeleo yangu mwenyewe binafsi na maisha yangu ninayoishi sasa hivi kila kitu kina chanzo na chanzo kinakuwa kina mmoja kwahiyo kupata kwangu mimi kuna mwingine nyuma yangu kwahiyo kila mafanikio yangu yana mtu nyuma kama ni mke kama ni bosi kama ni wafanyakazi wenzangu kama ni mama kama ni baba lakini yote ni maisha yangu mimi.


 EDNA WA AFM DODOMA:- Amigo kwanini ukija dodoma huzunguki redio nyingi kama wasanii wengine hii ni mara ya pili nimejaribu kutaka kufanya interview na wewe unaniambia upo bize ni kwamba unaenda kwa uliowazoea au inakuwa vipi au kukupata mpaka tuandike barua na takrima?.

 

 PRINCE AMIGO:- Bibie edna hujawahi kuniambia mimi hata siku moja, na nikifika dodoma huwa kwa niaba yaani tupo kikampuni zaidi kwahiyo sisi huwa tunaambiwa tunatakiwa tukafanye interview redio flani siwezi kukurupuka eti nizunguke redio zote inawezekana kweli! labda edna ulimpigia amigo mwingine sio amigo mimi.

 

       Jamani maswali yalikuwa mengi sana ila kwa leo naomba niishie hapa maana amigo alikuwa katika wakati mgumu mno kujibu maswali ambayo yalikuwa yakimiminika kama mvua, ila napenda nimpongeze sana amigo kwa ushirikiano mkubwa ambao aliuonyesha siku ile...tupo pamoja sana!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni