TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 2 Juni 2016

OMARY TEGO ATAMBULISHA WIMBO MPYA WA RAMADHAN KAREEM WENYE MAHADHI YA TAARAB.

NA KAIS MUSSA KAIS.


          Mkurugenzi wa coast modern taarab omary tego ameachia wimbo mpya kabisa uitwao "ramadhan kareem" ambao upo katika mahadhi ya taarab tokea jumatatu ya wiki hii.


OMARY TEGO MKURUGENZI WA COAST MODERN TAARAB.

        Akizungumza na mtandao huu omary tego alisema kwamba hii ni zawadi kwa waislam wote tanzania na nje ya mipaka ya tanzania, huu ni ukumbusho kwa waislam wenzangu juu ya mwezi huu wenye fadhira na radhi nyingi toka kwa mola wetu, huu ni mwezi wa toba  na upo mara moja tu kila mwaka tuepuke mambo yote yanayomchukiza mola wetu na tumsujudie mungu wetu kwa dhati kabisa kwani wapo ambao walipenda wapate bahati kama hii lakini mwenyezimungu alichukua pumzi zao, sasa wewe ukiwa mwenye afya na uwezo wa kumsujudia mola wetu kwanini usifanye hivyo? alihoji omary tego the special one!.


       Mtandao huu utawawekea wimbo huo hapa hapa ili muusikie na video pia itawekwa humu pindi itakapokuwa tayari imewasilishwa katika dawati letu ila kwa sasa tutawawekea ile coming soon ya video nayo mtaiona na kutoa maoni yenu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni