TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 3 Mei 2016

TOT MODERN TAARAB YA SASA NI MOTO WA KUOTEA MBALI

 NA KAIS MUSSA KAIS.

WAIMBAJI WA TOT TAARAB WAKIWA MAZOEZINI.

            Bendi ya Tot modern taarab kwa sasa wapo katika mazoezi ya nguvu kuandaa albam yao mpya ambayo mpaka sasa bado hawajaipa jina rasmi.


       Akizungumza na mtandao huu director wa bendi hiyo mbange alisema kuwa mpaka sasa tayari wameshafanikiwa kurekodi nyimbo nne ambazo ni:- 




                               1. usinishangae ulioimbwa na Abdul misambano
                               2. ukishangaa ya kwangu utachelewa kufanya yako, muimbaji ally star
                               3. muungwana haropoki muimbaji sharifa ketto
                               4. wala sikuopoi muimbaji aziza abdul "bonge"


       Tulikuwa tumekaa kimya kwa muda mrefu sababu tulikuwa katika mchakato mzima wa kampeni za uchaguzi mkuu, lakini sasa tumejipanga vyema ili kuleta ushindani katika tasnia hii ya taarab nchini tanzania, jambo la muhimu tunawaomba wapenzi watupokee kwani tukishamaliza maandalizi haya tutaanza kufanya show mwanzo mwisho hapa dar mpaka mikoani alimaliza kueleza director huyo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni