TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 2 Mei 2016

HASHIM SAID "IGWEE" AIPA KISOGO WAKALIWAO, KUNA TETESI YUPO NJIANI KURUDI MASHAUZI CLASSIC!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


HASHIM SAID "IGWEE" BONGE LA BWANA.

       Unaweza kukaa chini na kujiuliza kwani wakaliwao modern taradance kuna nini? mbona wasanii wanazidi kuhama kila kukicha? lakini jibu la swali hili wanalo viongozi wenyewe wa bendi ya wakaliwao chini ya mkombozi thabit abdul na meneja ally juma.


       Baada ya wiki mbili zilizopita msanii Aisha othman vuvuzela kuhama wakaliwao na kujiunga na jahazi modern taarab, leo hii tena kuna taarifa Hashim said "igwee" au unaweza kumuita bonge la bwana kuna tetesi anarejea mashauzi classic akiipa mkono wa kweli wakaliwao modern taradance, hii ni kama tamthilia yenye muendelezo wa scene!, mtandao huu ulipata taarifa za hashim said kurudi zake mashauzi classic yapata wiki mbili na nusu sasa na vikao vya siri vilikuwa vinafanyika, lakini tuliendelea kuzifanyia uchunguzi wa kina ili kujiridhisha.


     Lakini leo status ambazo amekuwa akiziandika hashim said mwenyewe kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii imekuwa ikitafsiliwa kuwa ni maandalizi ya yeye kurejea tena katika bendi yake ya zamani, moja ya status yake ambayo Hashim ameiandika katika mtandao wa kijamii facebook unasomeka hivi:- "yaliyopita yanakuwa si ndwele, waungwana huganga yajayo...babu alinambia...ushirikina ni kama koti likikubana livue...leo nalivua nyumbani...nyumbani ni nyumbani...mwenda kwao sio mtoro...ulimi hujaza mafaili ya kumbukumbu, kiapo changu ni uthibitisho tosha kwa matamshi yangu nazingatia nisije onekana sina maana baadae". Haya ni maneno ambayo ameyaandika yeye mwenyewe.


      Tuliamua kumtafuta Hashim kwa njia ya simu ili atuthibishie tetesi hizi lakini alipopatikana alisema siwezi kuongea chochote kwa sasa ingawa mimi ni mlengwa wa hili jambo ila muda utakapofika basi nitazungumza lakini kwa sasa sina la kusema kama kurudi nyumbani ndio tatizo! hata east african melody pia ni nyumbani sio mashauzi tu alimalizia kusema. tunawaahidi kumtafuta sumalager ambae ni meneja wa mashauzi classic ili atuthibitishie taarifa hizi ndugu wasomaji, kikubwa tuendelee kufuatilia na naamini majibu yatapatikana hapa hapa kama anaenda mashauzi classic au anarudi east african melody...tusubiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni