TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 2 Mei 2016

NANI ZAIDI KATI YA KONGAMOYO BENDI NA MATONAS G CLEF BENDI YA ZANZIBAR TAREHE 18/5/2016 NDANI YA LANGO LA JIJI MAGOMENI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

        Hii ni siku ambayo wapenzi na mashabiki wa taarab asilia "old is gold" watafurahi na roho zao kwa kushuhudia mpambano kati ya kongamoyo bendi watoto wa magomeni na matonas g clef bendi toka zanzibar siku ya jumatano ya tarehe 18/5/2016 katika ukumbi wa magomeni lango la jiji dar.


      Akizungumza na mtandao huu ambao hauna ubaguzi na bendi yoyote ya taarab nchini, mkurugenzi wa kongamoyo Igbal alisema kuwa hii ni siku maalum ambayo haijapata kutokea kwa kipindi cha muda mrefu sana hususani katika hii miondoko yetu ya "old is gold", tumejipanga kushusha burudani ya nguvu ambayo haitowachosha mashabiki na wata-enjoy sana kikubwa nawaomba wajitokeze kwa wingi siku hiyo ya tarehe 18/5/2016 ndani ya lango la jiji magomeni.

 

     Kwa upande wake mkurugenzi wa matonas g clef bendi toka zanzibar mohamed issa matona alijinasibu kwa kusema kuwa, tutavuka maji kuja dar es salaam kwa kazi moja tu kuja kuwaonyesha hawa kongamoyo kwamba taarab asilia inapigwa vipi!, tumedhamilia na tumejipanga vilivyo kukonga nyoyo za wakazi wa dar. mara nyingi sisi huwa hatubahatishi, naamini mpambano utakuwa mzuri kikubwa tuombe mungu siku ifike na pia nawaomba wapenzi waje kwa wingi tarehe hiyo alimaliza kwa kusema. katika show hiyo kiingilio cha mlangoni itakuwa ni shilingi elfu 6,000/= tu kwa mtu mmoja nyote mnakaribishwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni