TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 2 Mei 2016

WATANGAZAJI WA TAARAB WATOA TAMKO LAO KWA WASANII WANAOKATAA KUSHIRIKI MAHOJIANO KIKAANGONI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


          Watangazaji wa vipindi vya taarab redioni na runingani ambao wapo katika group la ubuyu wa taarab whatsap kwa pamoja wametoa tamko lao kwa wale wasanii ambao kwa namna moja ama ingine hukataa yale mahojiano ya live ndani ya "kikaangoni wiki hii" kwa makusudi hawatocheza nyimbo zao hewani.


        Wamefanya mjadala huo kwa muda mrefu na hii ni kwasababu kuna msanii mmoja nguli wa muziki huu wa taarab nchini "jina kapuni" kuwadengulia na kutoa sababu zisizo na mashiko kwao, huyu amezoea sana na amekuwa akitudharau sana sisi watangazaji wa mikoani, hii si mara ya kwanza kwani hata mimi kuna siku aliwahi kunikatia simu huku akiwa hewani wasikilizaji wakimsikiliza, kisa kuna swali nilimuuliza ambalo kwanza alianza kufoka kabla ya kukata simu.


     Mtangazaji mwingine akitoa ushuhuda wake alisema kuwa alimpigia simu msanii huyo muda wa asubuhi na kumtaarifu kuwa ifikapo jioni atampigia simu kwani ana interview na yeye nae alikubali, lakini ilipofika jioni kila nikimpigia simu alikuwa anaikata makusudi huku mimi nikiwa tayari nimeshawaeleza wasikilizaji kuwa tutakuwa na flani katika kipindi siku hiyo!, hii ni dharau ya wazi wazi kabisa!.


     Mtangazaji mwingine nae alisema kuwa wasanii wamekuwa wakiwadengulia sana kila wanapotaka kufanya mahojiano nao, na hii ni kwa sisi tu tulio mikoani, wanatuona kama takataka, hawatuthamini wala kutujali kabisa!, ila wanapokuja huku mikoani huanza kuturamba miguu ili tu tuwafanyie promo kwakuwa siku hiyo wanatumbuiza mkoani kwetu, sasa tunasema tumechoka kufanywa wa baadae! wanatulingia utafikili tunawaomba pesa bwana! maamuzi yetu yaheshimiwe, tunaomba ndugu admin ufikishe ujumbe wetu kwao ili watambue maadhimio yetu kwa pamoja.


       Group la ubuyu wa taarab whatsap limesheheni watangazaji wapatao 97 mpaka sasa tokea mikoa mbalimbali ya tanzania pamoja na nchini kenya, kila jumatatu kumekuwa na kipengele kiitwacho "kikaangoni wiki hii" hapo watangazaji kwa pamoja hupendekeza msanii wanaomtaka ili siku ya jumatatu admin aweze kumuingiza kwa group tayari kwa mahojiano ya "live" kati ya watangazaji hao na msanii husika, sasa kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakileta malingo pindi wanapofikishiwa ujumbe wa kutakiwa kuwepo katika kipengele hicho, hivyo watangazaji hao kwa pamoja wamefikia maamuzi ya kutocheza nyimbo za msanii yeyote ambae atakataa kujumuika nao tena bila sababu za msingi katika kipengele hicho. Jumatatu ya leo ilikuwa tuwe na black kopa ila mambo hayakwenda sawa tutakuwa nae kesho kwa maswali na majibu...Ahsanteni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni