TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 30 Aprili 2016

DOT DO:- SIKU ZOTE MAFANIKIO HAYAJI KWA MANENO NA MAJUNGU BALI HUJA KWA JUHUDI, MAARIFA NA VITENDO

NA KAIS MUSSA KAIS.


MKURUGENZI WA ALJAZEERA, MOHAMEDY SALM "DOT DO".

             Mkurugenzi wa aljazeera modern taarab "wataalam wa old is gold" mohamedy salim almaarufu "DOT DO" amesema mafanikio huja kwa vitendo na sio maneno maneno yasiyo na muelekeo.


         Aliyasema hayo jana wakati akiwasiliana na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya mtandao wa "imo" tokea oman alipo kwa sasa!, unajua mikakati yangu ambayo nimeifanya kwa bendi yangu ya aljazeera ni mikubwa sana na sasa naona wazi inakwenda kama ambavyo nimepanga, ingawa nipo mbali sipo tanzania lakini nimetumiwa video hapa ya umati ambao umehudhulia show yetu ya jana jumamosi hapo D.D.C. kariakoo mpaka nimechanganyikiwa kwa jinsi watu walivyokuwa wengi, hii inanipu moyo na hamasa kubwa ya kufanya mambo mazuri zaidi.

 

     Watu niliowaona ambao wamehudhulia show ile ya jana huko tanzania wengine sikutegemea kuwaona kabisa kabisa!, mimi nawaambia karibuni sana na raha ambazo mlizipata jana basi tegemeeni kuendelea kuzipata zaidi ya zile katika wiki lijalo kwani vijana wangu mazoezi kwao ni kitu muhimu ili kutengeneza nyimbo zingine nzuri ambazo hujawahi kuzisikia popote pale alimaliza kwa kusema, bendi hii ya aljazeera hufanya show zake kila jumamosi katika ukumbi wake wa nyumbani wa D.D.C. kariakoo siku za jumamosi, njoo ujionee mambo mazuri na muziki mtamu wa "old is gold" toka kwa vijana hawa wa aljazeera.


     

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni