TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 30 Aprili 2016

AISHA VUVUZELA NA ZUBEDA MLAMALI KUNEMA LEO MBELE YA MASHABIKI LUKUKI WA JAHAZI MODERN TAARAB.

NA KAIS MUSSA KAIS.


      Ile siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa jahazi modern taarab hatimae imefika, ni leo ndani ya ukumbi wa travetine magomeni wasanii aisha othman vuvuzela na zubeda mlamali watatambulishwa rasmi mbele ya wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo.


       Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo mfalme mzee yusuph alisema kwamba maandalizi yote kwa ajili ya shughuli hiyo yamekamilika, kikosi chote cha jahazi modern taarab kipo tayari kabisa kwa burudani, kilichobakia ni kungoja masaa yafikie ili tuwape raha wapenzi wetu katika utambulisho huo, wapenzi na mashabiki mia moja wa kwanza tutawapatia t-shirt bure za jahazi modern taarab na hii ni kuwaonyesha kuwa ni kwa kiasi gani tunawajali alisema mkurugenzi huyo.


       Kwa upande wake zubeda mlamali yeye alisema kwamba yupo vizuri kabisa na wapenzi watarajie vitu vizuri toka kwake siku hii ya leo. nae aisha othman vuvuzela alijinasibu kwa kusema kuwa siku zote huwa habahatishi, hapa kazi kazi tu! nawaomba wadau wajitokeze kwa wingi kwani hatutowaangusha kabisa, ikumbukwe kuwa kiingilio katika show hiyo ni shilingi elfu 8,000/= za kitanzania kwa mtu mmoja, milango itakuwa wazi kuanzia saa mbili kamili za usiku na nyote mnakaribishwa!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni