TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 3 Juni 2016

WATANGAZAJI WA TAARAB KUMALIZANA "KIKAANGONI" NA KHADIJA OMARY KOPA JUMATATU YA TAREHE 6/6/2016.

NA KAIS MUSSA KAIS.


        Watangazaji wa vipindi vya taarab kupitia runinga na redio mbalimbali afrika mashariki watamaliza ile awamu ya kwanza ya ile segment yetu ya kikaangoni wiki hii kwa kufanya mahojiano na malkia wa mipasho nchini khadija omary kopa siku ya jumatatu tarehe 6/6/2016 ndani ya group la whatsap la ubuyu wa taarab.


MALKIA WA MIPASHO KHADIJA OMARY KOPA.

      Akizungumza na mtandao huu khadija kopa alithibitisha kushiriki kikaango hiko na pia alichukuwa nafasi hii kuwaomba radhi watangazaji hao kwani ilikuwa awepo muda mrefu sana katika segment hiyo ila maandalizi ya uzinduzi wa bendi yake ya ogopa kopa yalimfanya awe bize sana khali iliyopelekea yeye kushindwa kushiriki, ila kwa sasa ameahidi kushiriki kujibu maswali bega kwa bega na watangazaji hao.


        Ikumbukwe baada ya mahojiano haya na khadija kopa segment hii itasimama ili kupisha mwezi mtukufu wa ramadhan ili waislam wafunge kwa utulivu na amani, baada ya kumalizika kwa mfungo huo mtukufu basi tutaendelea kama ilivyo ada yetu. wasomaji wa mtandao huu tusubili tuone malkia huyo atawaweza watangazaji hawa waliokuwa familia moja kwa sasa na wana ushirikiano wa hali ya juu katika maswali yao?, kikubwa tusubiri tuone!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni