Aljazeera old & modern taarab watoto wa kariakoo mtaa wa jangwani leo hii siku ya jumamosi wanatarajia kushusha burudani ya nguvu ndani ya ukumbi wa D.D.C. kariakoo hapa jijini dar es salaam.
Akizungumza na mtandao huu director wa bendi hiyo Abubakar mgeni alisema kwamba hii itakuwa ni show yao ya mwisho kabla ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhan ambao utaanza tarehe 7/6/2016 siku ya jumanne. kuna mambo mengi tumewaandalia wapenzi wetu siku hii ya leo naamini wata-enjoy sana, kuna nyimbo nzuri tumeziandaa kwa ajili yao jambo la msingi ni kwa wao kujitokeza kwa wingi siku ya leo alimaliza kwa kusema director huyo.
Aljazeera wamekuwa wakijaza sana watu kipindi hiki na kikubwa kinachowapa nguvu hii ni ubora wa kikosi chao kuanzia wapiga vyombo mpaka waimbaji, wamekamilika haswa burudani zote utazipata kuanzia za akina malika, fatma issa, makame faki, abdallah issa na nyinginezo nyingi sana, twende kwa pamoja leo tukawashuhudie vijana hawa wakifanya yao siku ya leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni