TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 5 Juni 2016

TETESI:- OMARY SOSHA KUJIUNGA NA ALJAZEERA OLD & MODERN TAARAB WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

OMARY SOSHA AKIWA KWENYE POZI.

         Muimbaji mwenye sauti ghali kwa sasa katika miondoko hii ya taarab asilia Omary sosha inasemekana yupo mbioni kujiunga na bendi ya aljazeera old & modern taarab wakati wowote ule kuanzia sasa.

        Habari za uhakika kabisa zilizofika ndani ya dawati letu la habari zinasema kuwa mazungumzo kati ya omary sosha na wakurugenzi wa bendi hiyo yameshafanyika na kinachofuata sasa ni utekelezaji tu kwani anasubiliwa mkurugenzi mwingine Jamali mperampera ambae kwa sasa yupo nje ya nchi atakapokuwa ameingia basi mara moja utekelezaji utafanyika juu ya msanii huyu.

      Omary sosha amekuwa akionekana mara kwa mara katika jukwaa la aljazeera akiimba na hata katika maharusi mbalimbali pia hushiriki na bendi hiyo, alipoulizwa omary sosha mwenyewe juu ya habari hizo kuzagaa alisema ni mapema mno kulizungumzia jambo hili kikubwa tuvute subira itakapokuwa issue imekamilika basi kila kitu kitakuwa wazi kwenu wandishi.ikumbukwe omary sosha alikuwa ni muimbaji wa dar modern taarab kabla ya kuacha na kuelekea washawasha bendi iliyo chini ya amour magulu ambae nae alitokea huko huko dar modern kabla ya kuanzisha bendi yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni