TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 8 Juni 2016

MZEE YUSUPH:- NAWATAKIA WAISLAM WOTE DUNIANI MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN.

NA KAIS MUSSA KAIS.

         Mkurugenzi wa jahazi modern taarab mfalme mzee yusuph amewatakia waislam wote duniani mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa ramadhan ambao umeanza siku mbili zilizopita.

        Akizungumza na mtandao huu mfalme mzee yusuph amesema kwamba hiki ni kipindi cha kumuabudu mwenyezimungu na kutimiza moja ya nguzo tano za kiislam, mwezi huu huja mara moja tu kwa mwaka hivyo yatupasa sote kwa pamoja kufunga na kutenda yalo mema ili kumpendeza mungu alisema.

         Kipindi hiki bendi zote za taarab zimesimamisha maonyesho yao kutokana na mwezi huu mtukufu wa ramadhan, nasi kwa upande wetu mtandao wa ubuyu wa taarab tunawatakia waislam wote mfungo mwema wa ramadhan tukufu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni