Mfanyabiashara na mdau mkubwa wa muziki huu wa taarab nchini Turiplety kais mwenye makazi yake oman na hapa nchini tanzania amesema kwamba kuna tofauti kubwa sana ya taarab asilia na taarab ya kisasa yaani taradance.
Alizungumza haya ndani ya holiday inn hotel maeneo ya posta wakati alipompa mwaliko mwandishi wa habari hizi kufuturu nae pamoja na kampani yake ya wafanyabiashara wenzake, akizungumza kwa msisitizo Turiplety alisema kwamba anakumbuka sana wakati yupo visiwani zanzibar alikuwa akiona raha ya taarab asilia, hakuna fujo, ustaarabu asilimia mia, watu wote waelewa, muziki unausikia kwa nafasi,muimbaji katulia, mashairi yanaeleweka yaani mpaka raha, ukijipulizia pafyumu yako nzuri basi utarudi ukinukia hivyo hivyo! watu wote wametulia katika viti, wimbo ukimfurahisha mshabiki ananyanyuka huku akicheza kwa madaha yaani taratibu na kwenda mbele kutunza kisha anarudi kukaa kitini mwake safi kabisa!.
Lakini hizi taarab za sasa kwanza muziki unakuwa upo spidi sana sasa muimbaji huwezi kumuelewa maana itamlazimu kuendana na spidi ya muziki unaopigwa sasa hapo utasikia au kuelewa nini? taarab hii inapoelekea haitokuwa tofauti na kisingeli muziki unaochezwa na vijana uswahilini, kiukweli inabidi wabadilike sana, mimi binafsi yangu huwezi kunikuta kwenye kumbi zao, nawapenda ila siendani na spidi zao kwakweli alimaliza kwa kusema mdau huyo.
Turiplety pamoja na kufanya biashara zake oman to tanzania lakini pia ni muigizaji wa michezo ya kuigiza yaani bongo movie na yupo katika kampuni ya pilipili entertainment mpaka sasa amefanikiwa kucheza movie zifuatazo:- Ghafla siku moja, C.I.D. Talaka, kivuli, Boss lady, The story na maskini wa heri, movie ya kivuli inaendelea kuonyeshwa katika chanel ya african magic Dstv na hii ya Talaka itaanza kuonyeshwa star tv kuanzia alhamisi ya wiki ijayo, huyo ndie Turiplety kais mdau wa taarab, muigizaji na mfanyabiashara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni