Na pambe za taarab. muziki wa taarab kwa muda mrefu sasa umekuwa kama mtoto yatima ambae ameondokewa na wazazi wake na asipate huduma toka kwa jamii inayomzunguka, ilipokuwa imesimamishwa kutoa huduma blog ya ubuyu wa taarab wasanii walikosa kwa kusemea mambo yao ndipo tulipokaa chini na kuzungumza na mmiliki huyo ambae ni kais mussa kais ili ikiwezekana atuuzie blog yake nasi tuendeleze pale alipokuwa ameishia.
Nashukuru alituelewa ila hakuwa tayari kutuuzia isipokuwa tutaiendesha blog hii kwa makubaliano maalum ambayo mpaka sasa ni siri baina yetu, isipokuwa tumebadili kutoka ubuyu wa taarab mpaka pambe za taarab, unaweza kushangaa humu ndani ukakuta habari ambazo kais mussa kais aliziandika kwa ubuyu wa taarab. ninachokiomba toka kwenu wadau ni ushirikiano na viongozi wote wa bendi za taarab wakati wenu ni huu sasa kutangaza muziki huu kupitia blog hii mpya ambayo tumeisambaza katika mitandao yote mikubwa duniani ili habari zetu ziwe zinaenea kwa urahisi.
Pambe za taarab inayo page yake ambayo wewe kama mdau ili kupata habari kiurahisi unatakiwa ku like page hii na kuendelea kuburudika na raha za pwani, ahsanteni sana na karibuni nyote.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni