Na pambe za taarab.
Zanzibar star's modern taarab bendi iliyoanzishwa upya chini ya mkurugenzi Juma mbizo siku ya jumanne ndani ya ukumbi wa DDC kariakoo walifanya show ya nguvu iliyowafanya wadau na wapenzi kutoa machozi ya furaha kwa kukumbuka enzi za bendi hiyo ilipokuwa ikifanya vizuri.
Show hiyo ambayo ilihudhuliwa na wapenzi tokea mikoa ya karibu ilikuwa ni ya kwanza rasmi baada ya kufanya ile ya pale dar live na mango garden ambapo walikuwa wasindikizaji tu. Show ilianza saa tatu kamili kama kawaida na wasanii wale nguli wa bendi hiyo enzi hizo walikuwepo. Bibie mwanahawa ally ndie aliongoza safu ya waimbaji wa zamani.
Katika show hiyo wasanii Mossi suleiman, zubeda mlamali, Mwamvita shaibu, khadija Yusuph, Issa kamongo, Zena mohamedy, Aisha masanja na mwaija zayumba walifanya mambo makubwa yaliyowafanya wapenzi kuchanganyikiwa kwa furaha.
Mtandao huu ulipata nafasi ya kuzungumza na mkurugenzi wa bendi hiyo Juma mbizo ambae alisema kwamba burudani hizo zitaendelea kwa siku hiyo ya jumanne bila kukoma, vile vile mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa tayari wameandaa show ambayo itazikutanisha zanzibar star's, Jahazi modern taarab, msagasumu, Kivurande junior na wasanii wengine wengi ambayo itafanyika katika ukumbi wa Dar live siku chache zijazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni