TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 6 Julai 2017

SUPERSHINE MODERN TAARAB, SINGELI, BAIKOKO KUNOGESHA USIKU WA MAMBO YA PWANI JUMATANO DAR LIVE.

Na pambe za taarab.

    Bendi kongwe ya supershine modern taarab yenye maskani yake magomeni jijini dar, jumatano ijayo wakishirikiana na singeli fleva, baikoko na kibaokata wanatarajia kufanya makubwa katika show iliyopewa jina la usiku wa mambo ya pwani kwenye ukumbi wa dar live mbagala jijini dar.

    Akizungumza na mtandao huu msemaji wa bendi hiyo Queen Salma alisema tumeamua kuwapa wapenzi wetu radha tofauti ili kufanya kila mmoja kuenjoy. Unajua tumefuata maoni ya wapenzi wetu wanaotaka kuona tunafanya burudani mseto.

   Bendi ya supershine huwa inafanya show hapo katika ukumbi huo wa dar live mbagala kila jumatano kwa kiingilio wanaume shilingi 5000 na wanawake shilingi 2000, wadau mnaombwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya jumatano ili kupata burudani roho inapenda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni