Na pambe za taarab.
Wakaliwao modern taradance chini yake mkurugenzi Thabit Abdul siku ya jumanne watakuwa na kibarua kigumu ndani ya ukumbi wa friend's conner watakapokuwa jukwaa moja na twanga pepeta kisima cha burudani.
Show hii itazima yale majigambo ya bendi zote mbili ambazo kwa nyakati tofauti walikuwa wakitamba. Kwa upande wake Ally choki alisema kuwa wakaliwao ni bendi changa sana ambayo haiwasumbui wala kuiwazia na siku hiyo tutawafundisha Muziki. Thabit Abdul alisema kuwa udhaifu wa twanga naujua wazi kabisa, mpaka sasa naona kama tumeshawakalisha hawana jipya twanga ilikuwa zamani enzi zetu lakini sio sasa hivi.
Wadau na wapenzi mnaombwa kujitokeza kwa wingi kwani kiingilio ni rahisi sana 8000 tu kwa mtu mmoja na show hiyo itasindikizwa na Mc sudi mzee wa singeli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni