TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 1 Januari 2018

HERI YA MWAKA MPYA WASOMAJI WOTE WA MTANDAO WA PAMBE ZA TAARAB.

Na pambe za taarab.

Katika kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya mtandao wa pambe za taarab unatoa pongezi kwa wasomaji wake kwa kuweza kufika salama ndani ya mwaka huu 2018.

Akizungumza kwa upole mkurugenzi wa Kampuni ya skillman media ambae ndio mmiliki wa mtandao huu bwana kais mussa kais alisema kuwa shukrani na pongezi ziende kwa mwenyezimungu kwa huruma zake na kutuchagua kuwa miongoni mwa tulioweza kufika ndani ya mwaka mpya! hata wale ambao wameingia 2018 wakiwa wagonjwa tunaomba kwa mwenyezimungu awape nafuu ili waweze kuendelea na harakati za ujenzi wa taifa.

Akizungumzia matarajio ya mtandao huu wa pambe za taarab kwa mwaka huu wa 2018 kais mussa kais alisema kuwa tutakuwa na maboresho makubwa hususani kiutendaji!, kuna vifaa vya kiutendaji tutaongeza, wafanyakazi tutaongeza na tupo katika mipango mikubwa ya kuiboresha zaidi ofisi yetu kikubwa tumuombe mungu aweze kutupa pumzi na ridhiki ya kuweza kuyatimiza haya yote tuliyoyapanga alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni