Na pambe za taarab.
Muimbaji anaetamba kwa sasa ndani ya bendi ya wajelajela iliyopo visiwani zanzibar Mwinyimkuu ameibuka na wimbo wake mpya kabisa uitwao sweet of my heart ambao ktk video yake amemshirikisha Husna hassan chitoto kama video Queen. Husna ni muimbaji wa bendi hiyo lakini pia ni mke mtarajiwa wa Mwinyimkuu baadae ya kupigana kibuti na Maina thadei aliekuwa mkewe.
Akizungumza na mtandao huu makini Mwinyimkuu alisema huu ni wimbo mzuri sana na itapendeza kwako mdau kama utatembelea mtandao wa www.wasafi.com kutazama video ya wimbo huu kwani location yake sio mchezo ni wimbo mzuri sana naomba mnipe sapoti. Alipoulizwa kuwa huu wimbo kamuimbia Husna chitoto ili kumrusha roho Maina thadei? Mwinyimkuu alikataa akasema kuwa huu ni wimbo kama nyimbo zingine ambazo zina ujumbe unaogusa jamii sikuimbia Husna wala sikuwa namrusha roho Maina thadei hapana siwezi kufanya kitu kama hicho brother.
Unajua kuachana katika mapenzi ni jambo la kawaida tu na sisi sio wa kwanza kuachana, kwa sasa kila mmoja ana maisha yake na kila mmoja ana mahusiano ya kimapenzi na mwingine hivyo maisha yanaendelea sioni kama kuna tatizo hapo. Mwinyimkuu baada ya kuondoka katika bendi yake ya zamani ya excellent iliyopo dar es salaam alijiunga na bendi ya jeshi la magereza ambayo ipo zanzibar ambayo inafahamika kama wajelajela original na yupo hapo mpaka sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni