Na pambe za taarab.
Muziki wa taarab nchini unaonekana kupoteza ile hamasa na msisimko uliokuwepo zamani na hii haswa ni baada ya mfalme mzee yusuph kumrejea mungu na kuachana kabisa na masuala ya muziki huu wa taarab.
Wapenzi na mashabiki kadhaa walijitokeza hadharani mbele ya ofisi za mtandao huu na kutaka kujua ni nani anafaa kurithi nafasi ya ufalme kati ya prince amigo na omary tego!, unajua wawili hawa kwa sasa ndio kioo katika bendi zao na wapenzi wanataka kufahamu nani zaidi baina yao!. Akijinasibu prince amigo alisema kwamba mimi ndio mtoto wa mfalme na alipoacha muziki ameniagiza mimi kurithi mikoba yake na nipo mpaka sasa katika nafasi hiyo na sitorudi nyuma.
Omary tego kwa upande wake alisema kuwa Amigo ni mtoto mdogo na sidhani kama cheo cha ufalme kinamfaa!, mimi ndio mwenyewe sahihi kuchukuwa cheo hicho ili niweze kuendeleza taarab nchini Tanzania alimaliza kwa kusema omary tego.
Wadau wa taarab wamekuwa wakipata wakati mgumu sana mpaka wakati mwingine kurushiana ngumi kwa mabishano ni nani mfalme wa kweli kwa sasa katika taarab, jibu naamini mnalo ninyi wasomaji wangu na mtafunguka hapo chini kwa maoni yenu juu ya issue hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni