TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 10 Januari 2018

ZAINAB MACHUPA AITOSA FUNGAKAZI RASMI, ATANGAZWA KUJIUNGA NA YAH TMK MODERN TAARAB.

Na pambe za taarab.

Muimbaji wakutegemewa wa fungakazi modern taarab Zainab machupa "sheshibeshi" ambae pia ni mke wa mkurugenzi Kapten temba siku ya jumatano ndani ya ukumbi wa burudani wa dar live mbagala alitangazwa rasmi kuwa ni muimbaji mpya wa yah tmk modern taarab.

Akimtangaza muimbaji huyo, Omary tego alianza kwa kusema napenda niwatangazie rasmi kuanzia leo kuwa muimbaji Zainab machupa rasmi ni msanii wa yah tmk modern taarab na tutaendelea kuwa nae katika show zetu zote, na nampandisha jukwaani rasmi na atatuimbia wimbo wa "kama wema unauzwa", baada ya kutangazwa Zainab alipanda na kuimba kwa ustadi mkubwa huku dada yake Ashura machupa akipanda stejini na kumtunza pesa mdogo wake.

Baadae mwandishi wa habari hizi alipata nafasi ya kuzungumza na Zainab machupa mwenyewe na kukili kwamba ni kweli kwa sasa yeye ni muimbaji wa yah tmk modern taarab na akaomba wadau, viongozi na wasanii wa bendi yake hiyo mpya kumpa ushirikiano ili kuiendeleza mbele zaidi bendi hiyo, alipoulizwa sababu za kuitosa bendi ya mumewe fungakazi na kujiunga na yah tmk, Zainab machupa alisema kuwa hii ni kazi nimeamua kubadili upepo ili kupata changamoto zaidi.

Nae mkurugenzi msaidizi wa yah tmk modern taarab Shomari mwambala alisema tumeamua kumuongeza kundini Zainab machupa sababu ni muimbaji mzuri na ana kipaji cha hali ya juu naamini  ataisaidia sana bendi yetu akishirikiana na wasanii wenzie, kikubwa tunataka tuone juhudi zake katika kazi basi, hayo mambo mengine inabidi atuachie uongozi alimaliza kwa kusema Shomari mwambala.

Mwandishi wa habari hizi ulipiga simu ya mkurugenzi wa fungakazi modern taarab Kapten temba je ana maoni gani juu ya uamuzi uliofanywa na mkewe wa kuhamia yah tmk na kuitosa fungakazi yeye kama mkurugenzi anasemaje? lakini  kwa bahati mbaya hakupatikana hewani hivyo tunawaahidi wasomaji wetu kuwaletea maoni ya temba siku chache zijazo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni