Na pambe za taarab.
Waswahili wanasema ukisema cha nini, kuna watu wanasema watakipata lini?, hatimae mtalaka wa Mwinyimkuu aitwae Maina thadei pichani amepata mchumba alietambulika kwa jina moja tu la Hussein na tayari hatua za awali zimeshafanyika mpaka barua ya majibu na pesa za mahari zimelipwa na ndoa itafanyika mwezi wa tatu hapa hapa jijini dar es salaam.
Mwandishi wa habari hizi alipata bahati ya kukutana na wachumba hao maeneo ya mwembechai magomeni na kupiga nao stori mbili tatu juu ya maandalizi yao katika sherehe hiyo. Kwa kuanza Maina alimshukuru mungu na kusema kila linalokutokea ktk uso huu wa dunia yakupasa umshukuru mungu kwani wakati mwingine anakuwa na sababu zake!, mimi sijutii kuachana na Mwinyimkuu kwa maana naamini ridhiki ilikuwa imekwisha na lazima iwe vile, kwa sasa nipo katika maandalizi ya ndoa yangu na laazizi wangu Hussein kama unavyomuona mwenyewe handsome hana neno nampenda sana!, yamezungumzwa mengi sana baada ya mimi kutengana na Mwinyimkuu lakini yote namuachia mungu sababu mimi si muongeaji ila Mwinyimkuu mwenyewe anajua nini sababu kuu yakuachana kwetu.
Namuomba mungu aniwezeshe kufikia tarehe ya ndoa yangu nikiwa salama na mzima wa afya ili niwe mke halali na maisha yaendelee alisema Maina thadei huku akicheka kwa furaha. Kwa upande wake Hussein ambae ndie mume mtarajiwa wa Maina alisema, nampenda sana Maina tena nampenda mno! Maina ni mwanamke muelewa na msikivu naamini tutakuwa na maisha yenye furaha na amani wakati wote namuomba mungu atufanyie wepesi katika hili. Tukishafunga ndoa tunatarajia kwenda nairobi fungate ndivyo kamati imependekeza hivyo baadae tutarejea dar, tulipomuomba tupate picha yake alikataa akasema mimi sio wa mitandaoni sana mkitoa picha ya mchumba angu Maina inatosha sana tu alisema huku akiwa ni mwenye wasiwasi wa kupigwa picha ya kushtukiza.
Mwinyimkuu na Maina thadei waliowana na maisha yao yalikuwa ni mfano wa kuigwa kwa wapendanao, lakini mwishoni mwa mwaka jana ndoa yao ilivunjika ghafla na Mwinyimkuu kuanzisha mahusiano mengine na muimbaji wa bendi ya magereza zanzibar aitwae Husna hassan chitoto, lakini kwa upande wa Maina alikuwa kimya mpaka leo tunapojua kuwa yu mbioni kuolewa. Mtandao huu unamtakia Maina thadei maandalizi mema ya sherehe yake hiyo ya ndoa na mungu awabariki sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni