Na pambe za taarab.
Gazeti lako pendwa la mwanasoka kuanzia alhamisi ya wiki ijayo litakuwa na habari za taarab ambazo zitakuwa zikiripotiwa na mtandao huu chini ya wandishi wake mahiri kabisa.
Akizungumza mkurugenzi wa Kampuni ya skillman media ndugu kais mussa kais alisema kuwa utaratibu huu utaendelea pia katika redio kadhaa ambazo nazo zimeleta maombi ya kutumia habari ambazo zimekuwa zikiripotiwa na mtandao huu bora kwa sasa. Unajua mwanzoni baadhi ya redio zilikuwa zikiripoti habari zetu pasipo ruhusa toka kwa uongozi wetu lakini baada ya kuamua kusambaza barua katika redio mbalimbali juu ya katazo la kutumia habari zetu naona sasa wametuelewa alisema mkurugenzi huyo.
Gazeti la mwanasoka huwa linatoka kila siku ya alhamisi na jumapili, lakini habari za taarab utazipata siku ya alhamisi tu ndani ya gazeti hilo la michezo tunategemea wasomaji wetu tutakuwa pamoja kama ambavyo tunakuwa ndani ya mtandao wetu wa pambe za taarab.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni