Na pambe za taarab.
Kwa mujibu wa takwimu sahihi ambazo zimefanywa na mtandao huu bora wa taarab kwa sasa nchini Tanzania, bendi ya Yah tmk modern taarab inaongoza kwa ubora kati ya bendi tatu ambazo ni Yah tmk yenyewe, wakaliwao modern taradance pamoja na jahazi.
Kushika namba moja kwa yah tmk haikuwa rahisi kwani mchuano kati yao ulikuwa mkali sana ili kupata mshindi sahihi, vigezo vilivyotumika kupata washindi ni ubora wa nyimbo, uhai wa bendi nikimaanisha katika kufanya show's kwa wiki, kukubalika kwa bendi nikiwa na maana pale pindi bendi inafanya show muitikio wa mashabiki unakuwaje na mwisho kabisa ni nidhamu ya wasanii wanapokuwa stejini. Mtandao huu uliunda jopo la watu sita ambao walikuwa wakitembea katika kila kumbi ambazo bendi hizi zilikuwa zikifanya show zao tena bila wao kujua lolote kwamba kuna jambo kubwa linafanywa.
Katika majibu ya takwimu hii yaliyo wasilishwa katika dawati letu la habari siku ya jumatano iliyopita majibu yalikuwa ni kama ifuatavyo:-
1.Yah tmk modern taarab.
2. Jahazi modern taarab.
3. Wakaliwao modern taradance.
Bendi hizi tatu kwanza ndizo zenye uhai kwa sasa na wanafanya show zao kila wiki tena kwa kiingilio cha mlangoni, zipo bendi kama zanzibar stars modern taarab na ogopa kopa hizi hazijawekwa katika mchakato huu sababu mfano ogopa kopa wenyewe hawana show ya kila wiki isipokuwa inatokea tu mara moja moja wasanii wake wamekuwa wakionekana katika bendi zingine wakiimba ili kujipatia ridhiki, wenyewe wakiita style hiyo "ndondo". zanzibar stars modern taarab naweza kusema wamebakiwa na show moja tu ya pale Maisha basmet kila alhamisi kwani ile show waliyokuwa wakiitegemea pale D.D.C kariakoo imekufa baada ya kuwa wakizuiliwa kila mara na jeshi la polisi kulingana na sheria ya nchi, hivyo bendi hizi zikawa zimekosa sifa ya kuingizwa katika mchakato huu.
Jambo kubwa lililofanya mpaka bendi ya Yah tmk modern taarab kushinda ni uhai wa show zao mbili matata sana ambazo zimekuwa gumzo kwa kujaza watu tena kwa kiingilio cha mlangoni ambazo ni pale Dar live mbagala na Buriyaga bar iliyopo Temeke mwisho jijini dar, katika show hizi wadau, mashabiki na wapenzi wa taarab wamekuwa wakijitokeza kwa wingi mno, wasanii wa bendi hii wapo smart sana, wasafi na hukuti muimbaji amevaa kijora labda iwe show maalum ambazo hufanyika na kupewa jina "usiku wa vijora" wana nidhamu ya hali ya juu na kwenye live paformance utawapenda wapo vizuri mno, wapigaji wao vyombo ni wale wale huwezi kukuta sura mpya kama zilivyo bendi zingine hii inaleta chachu ya kufanya vizuri kwenye upigaji kwakuwa wamezoeana, kiusanii hii ina faida kubwa sana.
Mtandao huu unatoa pongezi kwa bendi ya yah tmk modern taarab na kuwaomba waendelee zaidi kuboresha wanapoona kuna mapungufu ili kufanya muziki wa taarab uendelee kupendwa kama zamani, bendi za Jahazi modern taarab na wakaliwao modern taradance wafanyie marekebisho kidogo mapungufu ambayo wanayaona katika safu zao za wapiga vyombo na waimbaji, lakini yote kwa yote kwa sasa hizi ndizo bendi ambazo unaweza kwenda kuangalia show zao na ukarudi ukiwa umeridhika na kufarijika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni