TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 15 Januari 2018

MWINYIMKUU:- HATA KAMA NITAALIKWA SIWEZI KWENDA KATIKA HARUSI YA MAINA THADEI.

Na pambe za taarab.

Muimbaji wa kutegemewa wa magereza modern taarab wana wa jelajela tokea visiwani zanzibar Mwinyimkuu amesema kamwe haitowezekana kwa yeye kuhudhulia harusi ya mtaraka wake Maina thadei hata kama atapewa mualiko.

Akizungumza kwa njia ya simu tokea visiwani zanzibar, mwinyimkuu alisema unajua shughuli ya Maina kama kweli ataolewa ni lazima itakuwa weekend nami kuanzia siku za alhamisi, ijumaa, jumamosi na jumapili bendi yangu ya magereza huwa tunakuwa na show, sasa siwezi kuacha sehemu inayonipa kula alafu nikahudhulie sherehe za ndoa itakuwa kituko kikubwa. Mimi sina neno na Maina tumeachana kwa amani na namtakia mafanikio katika hiyo ndoa yake ambayo atafunga!.

Alipoulizwa je kama atatokea mtu akawaunganisha katika kazi upo tayari kufanya wimbo wa pamoja na Maina?, Mwinyimkuu alijibu katika hilo hakuna tatizo sababu hiyo ni kazi na sio mapenzi. Maina thadei na Mwinyimkuu walioana ndoa halali kabisa ya kislam na walidumu ndoani takribani miaka kadhaa kabla ya kuvunjika katikati ya mwaka jana, kwa sasa Mwinyimkuu ana uhusiano wa kimapenzi na muimbaji mwenzie tokea hapo hapo magereza aitwae Husna hassan chitoto nae Maina ana uhusiano na mwanaume mwingine alietambulika kwa jina moja la Hussein ambae ndie anaetaka kumuoa nwaka huu ifikapo mwezi wa tatu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni