TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 16 Januari 2018

JUMANNE ULAYA MGUU NJE MGUU NDANI JAHAZI MODERN TAARAB.

Na pambe za taarab.

Mpiga gita la solo maarufu sana katika tasnia yetu ya muziki wa taarab nchini Jumanne ulaya "vidole vya biashara" ambae kwa sasa yupo bendi ya jahazi modern taarab amezinguana na uongozi wake na sasa takribani wiki ya pili haendi kazini, sababu kubwa ni malimbikizo ya madeni ambayo Jumanne anadai kwa viongozi.

Mtandao huu ulipopata taarifa hizi uliamua kumtafuta msanii huyo kwa njia ya simu ili aweze kuzungumzia sakata hilo je kuna ukweli wowote? nae alijibu kama ifuatavyo. Unajua mimi nimeingia nao mkataba jahazi tokea tarehe 23/11/2016 kwa makubaliano maalum ambayo yataendelea kubaki siri baina yangu na uongozi lakini tokea nisaini hawajawahi kunipa kile kiwango ambacho tuliahidiana kama malipo katika kila show tunazopiga, nikijaribu kuwakumbushia haki yangu hakuna jibu la maana ninalojibiwa, sasa mimi muziki ndio kazi yangu nina familia kubwa inanitegemea wasiponilipa stahiki yangu unadhani mimi nitaendeshaje maisha? alihoji msanii huyo.

Kwahiyo mimi sitokwenda kazini mpaka pale uongozi wangu utakaponilipa pesa zangu zote ambazo zinafika milioni tatu maana ni malimbikizo tokea mwaka 2016 alimaliza kwa kusema jumanne ulaya. Bendi ya jahazi modern taarab kwa sasa ipo chini ya bodi ya wakurugenzi watano ambao wanaiendesha, mtandao huu unawaahidi wasomaji wake kwamba  tutawatafuta viongozi wa jahazi modern taarab ili kuweza kujibu tu humu hizi wanazoshushiwa na msanii wao jumanne ulaya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni