TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 24 Oktoba 2014

OMARY KISILA:- MA-DIRECTOR NDIO TUNAOSHUSHA MUZIKI WA TAARAB NCHINI.

NA KAIS MUSSA KAIS

                 Jina la Omary Kisila sio jina geni katika tasnia ya muziki wa taarabu hapa nchini tanzania. Kisila ni Director wa bendi ya G5 Modern Taarab yenye maskani yake mtoni kwa Azizi Ally jijini Dar. katika kufikia mafanikio aliyonayo, Ommy Kiss amepitia bendi kadhaa kama zanzibar star, T motto, Diamond ya znz, Fungakazi na nyinginezo ambazo sijazitaja.

          Kwa kujua umuhimu wa kisila katika muziki huu, mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com ulimtafuta ili kutoa maoni yake ni wapi unapoelekea muziki wetu ukilinganisha na enzi zile za zamani?, Kisila ambae kitaaluma ni mpigaji wa kinanda na gitaa la Bess alikuwa na haya ya kusema

   Unajua sisi waongozaji wa muziki huu yaani madirector ndio ambao tunaurudisha nyuma muziki wetu kwa kukubali kuwatengenezea nyimbo wasanii ambao hawajafikia level ya kuimba taarab, yaani hawajui kabisa, na hii inasababishwa na hali ngumu ya maisha tuliyonayo. mfano mimi naweza kukataa kumtengenezea nyimbo msanii ambae hana kiwango, lakini msanii huyo huyo atakwenda kwa Director mwingine na atatengenezewa bila kujali ubora wa msanii husika.

     Hii ni mbaya sana sababu mwisho wa siku nyimbo zinakuwa hazina ubora na hazikai sana ktk soko la ushindani, ushauri wangu kwa viongozi wenzangu wa muziki huu, hebu tubadilike na tuweke vigezo vya ubora kwa msanii yeyote ambae atahitaji kutengenezewa wimbo au nyimbo na sisi Madirector!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni