TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 31 Oktoba 2014

OMARY ZUNGU:- WAKONGWE MJIPANGE, NIMEPANIA KUWAPOTEZA!.

NA KAIS MUSSA KAIS

               Omary Zungu, ni jina ambalo halijazoeleka sana katika tasnia yetu ya muziki wa taarabu hapa nchini tanzania,
OMARY ZUNGU
kijana huyu asili yake ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga. Shughuli za usanii alizianza tokea akiwa huko tanga kabla ya kuamua kuja Dar kutafuta maisha zaidi.


             Kwa sasa Omary Zungu ndie mpiga kinanda namba moja katika bendi ya Ogopa Kopa Classic Bend!. Alipofika Dar moja kwa moja alijiunga na bendi ya TOT ambayo anaitumikia mpaka muda huu pindi bendi inapokuwa na kazi. Mpaka sasa Omary Zungu amesharekodi nyimbo mbili akiwa na Ogopa Kopa ambazo ni Full Kuenjoy iliyoimbwa nae Black Kopa na Mamaa Mukubwa iliyoimbwa nae Malkia wa mipasho nchini tanzania Khadija Omary Kopa.


        Nilimuuliza amejipanga vipi ili kukabiliana na wakongwe katika tasnia yetu hii ya taarabu nchini?, alijigamba na kujisifu kwamba yeye amekuja kikazi zaidi, kwahiyo wanaojiita wakongwe wajiandae nakuja kivingine kabisa., sina mchezo kabisa. Huyo ndie Omary Zungu kibodi.

Maoni 1 :