Hemedy Omary ni mtunzi bora wa nyimbo za taarabu hapa nchini na tayari ameshatunga nyimbo nyingi sana ambazo zinaendelea kufanya vizuri, wasanii ambao tayari ameshawatungia nyimbo na zikafanya vyema ni Isha Ramadhan "mashauzi" wimbo wa Mama nipe radhi, Kila mtu na mtuwe, Baraka za Baba na Nani kama Mama, wengine ni Hanifa Maulidi Jike la Chui wimbo wa naufunga mtaa,
HEMEDI OMARY "SONARA WA MANENO". |
Hemedi Omary ana wimbo wake ameimba mwenyewe unafanya vizuri sana katika redio mbalimbali hapa nchini tanzania ambao unaitwa Sitaki mapenzi ya facebook na kuanzia wiki ijayo anatarajia kuanza kuifanyia shooting ili wadau na wapenzi wake waweze kupata video yenye ubora mkubwa.Sasa hivi Hemedi Omary yupo katika bendi ya Ogopa Kopa lakini pia bado ni muajiriwa wa kundi zima la TOT TAARAB!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni