TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 1 Novemba 2014

WAKALIWAO MODERN TARADANCE KUTAMBULISHA NYIMBO MBILI LEO!.

NA KAIS MUSSA KAIS

               Bendi ya Wakaliwao Modern Taradance chini yake Thabit Abdul au ukipenda muite Mkombozi leo wanatarajia kutambulisha nyimbo zao mpya mbili ambazo zitakuwepo katika albam yao ambayo wanatarajia kuizindua mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.

THABIT ABDUL "MKOMBOZI"
          Akizungumza na mtandao huu makini Thabit alizitaja nyimbo zenyewe kuwa ni Jasho la mnyonge hulipwa na mola ulioimbwa nae mkombozi mwenyewe, na wimbo wa pili  unaitwa Kumbe ndiyo tabia yako umeimbwa na chipukizi anae kuja kwa kasi, jina lake ni Nasra Shabban.

       Thabit alisisitiza kuwa safari hii ni lazima waungwana wamuelewe maana nyimbo zimesimama kupita kiasi na huyu chipukizi ni zaidi ya wakongwe. Wakaliwao ni bendi inayotikisa jiji na Tanzania kwa ujumla, kwa muda mchache tokea ianzishwe imepata mafanikio ya haraka mpaka kufikia kuteuliwa kushiriki tamasha kubwa kabisa la taarab nchini linaloandaliwa na kituo cha redio cha times fm 100.5, kupitia kipindi chake cha mitikisiko ya pwani kinachorushwa hewani kila jumatatu mpaka ijumaa saa sita mchana hadi saa kumi jioni na mtangazaji wako mahiri Dida.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni