TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 2 Novemba 2014

TAARABU ASILIA INAPOTEA, WADAU NA WAPENZI NINI TUFANYE KUUOKOA MUZIKI HUU?.

NA KAIS MUSSA KAIS

                  Nakumbuka wakati nipo shule ya msingi enzi hizo japo sio zamani sana msanii alienifanya nikaipenda Taarabu si mwingine bali ni Bibie Malika toka mombasa. Msanii huyu kiukweli aliitikisa haswa ukanda huu wa afrika mashariki na kati kwa vibao vyake murua na vyenye ujumbe mzuri.

BI SAADA MOHAMEDY
            Enzi hizo kulikuwa na wasanii wengine pia kama Juma ballo, Issa matona, Bi Sihaba Juma, Bi Saada Mohamedy na wengineo wengi wakifanya vizuri kwa nyimbo nzuri kupitia vikundi vyao tofauti tofauti, Taarabu asilia ilikuwa habari ya mjini asikwambie mtu! watoto, vijana mpaka watu wazima walikuwa wanapenda Taarabu sababu ndio muziki wa kistaarabu, hauna fujo wala kelele, unasikiliza na kucheza taratibuuu!.

BI SIHABA JUMA
         Sasa hivi ile radha halisi ya muziki huu inapotea imebakia visiwani zanzibar tu!, huku kwetu Bara hakuna kwakweli zaidi ya zile bendi zinazoitwa gusagusa zenyewe zinapiga kopi ya nyimbo za zamani lakini ukisikiliza kwa makini hizo nyimbo zinakuwa na mapungufu mengi. Huku ndipo ilipozaliwa hiyo mnayoiita modern taarab na modern taradance kwahiyo nawaomba wadau na wapenzi wote kuuenzi muziki huu na kuufanya usije ukapotea kabisa.



WAZEE WAKIPIGA VYOMBO VYA ASILI
          Bendi ziwe zinapiga japo nyimbo mbili au tatu za taarab asilia ili kuuenzi muziki huu na kuufanya usije ukapotea kabisa, waswahili wanasema ukipata chungu kipya usitupe cha zamani. Wadau tuamke wakati ni huu!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni