TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 2 Novemba 2014

ISHA MASHAUZI AWAPAGAWISHA WAKAZI WA BAGAMOYO NDANI YA UKUMBI WA EAGLE NEST!.

NA KAIS MUSSA KAIS

             Bendi ya Mashauzi Classic iliyo chini ya Mkurugenzi Isha Mashauzi, jana jumamosi ilishusha burudani ya nguvu ndani ya ukumbi wa Eagle Nest bagamoyo na kufanya wakazi wa maeneo hayo na vitongoji vyake kupagawa na kuomba burudani iendelee zaidi na zaidi.

KASSIM MGANGA NA ISHA MASHAUZI WAKIWAPA RAHA WAPENZI WAO.
          Katika onyesho hilo ambalo Mashauzi walisindikizwa na Kassim Mganga ukipenda muite Tajiri wa Mahaba ambae aliwachanga vimwana wa bagamoyo na kuwafanya walipuke kwa mayowe huku wakimshangilia kwa nguvu zote.Isha aliimba nyimbo tano mfululizo bila kushuka steji na pia alitambulisha wimbo wake mpya kabisa uitwao Sura su rambi, sura si roho, Nyimbo zingine alizoimba Isha Mashauzi ni pamoja na Mapenzi hayana dhamana, Asiekujua hakuthamini, Siwasujudii viwavi jeshi na Mama mashauzi.

KASSIM MGANGA NA ISHA MASHAUZI WAKIPOKEZANA KUIMBA.
Bendi yako ya Mashauzi Classic ni bendi bora kabisa kwa sasa ambayo inafanya vizuri kupitia nyimbo zake kadhaa wa kadhaa, kumbuka kila alhamisi bendi hii huwa inafanya show katika ukumbi wake wa nyumbani wa mango Garden kinondoni kwa kiingilio chako cha elfu tano tu nyote mnakaribishwa.


ISHA MASHAUZI AKIIMBA NDANI YA BAGAMOYO JANA.

WAPENZI WA MASHAUZI CLASSIC WAKISEREBUKA

KASSIM MGANGA AKIIMBA NA ISHA MASHAUZI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni