Taarabu ni muziki wenye asili ya pwani, muziki huu hapo zamani ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kuburudisha na kukufanya usahau machungu ya kutwa nzima kama ulikuwa shambani au ulikuwa katika kazi za ofisini. katka miaka ya 1960 taarabu ilishamili sana huko tanga na sehemu kadhaa wa kadhaa katika ukanda huu wa pwani ya mashariki.
Mipasho katika taarabu haikuanza leo, ilikuwepo tangia enzi za wazee wetu, lakini mashairi waliyokuwa wanayatumia yalikuwa yanaficha maana hususani kwa asiejua maana! mtu anafumbiwa wala wa jirani yako hajui kama kuna mtu kasemwa, rusharoho ilikuwepo lakini sio ya kutiana vidole vya macho kama ilivyo kipindi hiki.
MADADA WAKIAMULIWA UGOMVI. |
Maadili na ile miiko ya uandishi wa mashairi, uimbaji mpaka utengenezaji wa muziki wenyewe umejaa hasama na majibizano ya waziwazi kiasi kwamba hata mtoto wa darasa la kwanza hapati tabu kujua hapa kaimbwa fulani, Utamu wa Taarabu unapotea kwa kisingizio eti tunakwenda na wakati!, wakati gani huo? au ni huu wa kuiga tabia na hulka za kimagharibi?.
Sasa hivi ni kawaida sana tu kwa watu kugombana mpaka kufikia kupasuana eti kisa ni huu muziki wetu wa taarabu, utasikia ananirusha roho, sikubali mimi!, haya yametoka wapi? kwani hata zamani enzi za mabibi zetu hakukuwepo na mapenzi?. Ngumi hadi kwenye taarabu za vichochoroni ni kitu cha kawaida tu, mnapoteza ile radha halisi ya muziki wetu jamani. Nawaomba tubadilike ili tuupe thamani endelevu huu muziki wetu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni