TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 3 Novemba 2014

KULIKONI, MUSSA MIPANGO HAONEKANI KATIKA SHOW ZA JAHAZI MODERN TAARAB?.

NA KAIS MUSSA KAIS

                  Unapozungumzia wapiga magita ya bess hapa nchini tanzania hususani katika tasnia yetu ya taarabu!, basi ni lazima jina la Mussa Mipango utalitaja!, kwa sasa yeye ndio mpigaji bora wa gita hilo na yupo na bendi ya Jahazi Modern Taarab wana wa Nakshi Nakshi.

MUSSA MIPANGO AKIWAJIBIKA
              Takribani wiki tatu sasa amekuwa haonekani katika show za bendi hiyo, jambo lililopelekea wasomaji wa Blog hii kupiga sana simu katika chumba chetu cha habari wakitaka kujua kulikoni tena mpaka kipenzi chao hawamuoni katika show?, na huku wamekuwa wakipishana nae mitaani akionekana ni mwenye afya njema wala haumwi!,

            Kama kawaida ya ubuyuwataarabutz.blogspot.com kufuatilia habari kwa kina ndipo tulipompigia simu meneja wa Jahazi Modern Taarab Hamisi Boha ili kupata undani wa sintofahamu hii, Yeye alijibu kwamba Mussa Mipango alikuwa anaumwa ndio sababu zilizopelekea hata safari ya mikoani kutokwenda nae, lakini hakuna tatizo lolote lingine nawaomba wapenzi wetu wa Jahazi Modern Taarabu

MUSSA MIPANGO KUSHOTO, MZEE YUSUPH KATIKATI NA MOHAMEDY MAUJI KULIA WAKIWAPA RAHA MASHABIKI WA JAHAZI MODERN TAARABU.
waelewe hivyo.

        Tulipompigia simu Mussa Mipango yeye alijibu kwa sasa nipo hapa hospitali ya temeke, mdogo wangu wa kiume anaumwa amelazwa hapa, sitoweza kulizungumzia suala hilo kwa sasa namuhangaikia mgonjwa kwanza mpaka nijue hatma yake, tumezaliwa wawili tu, mimi na mdogo wangu huyu wakiume kwahiyo hii hali ya kuumwa kwa mdogo wangu imenichanganya, naomba unipe muda tutazungumza wakati mwingine.

         Mtandao huu unakuahidi kufuatilia kwanza taarifa za yeye kutoonekana kazini na jambo la pili kujua zaidi juu ya afya ya mdogo wake alielazwa hapo hospitali ya temeke inaendeleaje.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni