TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 28 Oktoba 2014

QUEEN SALMA:- USIA WA BABA NILIUTUNGA KWA HISIA KALI SANA!.

NA KAIS MUSSA KAIS

              Kwa sasa imekuwa ni fashion kwa bendi nyingi za taarab hapa nchini kutunga nyimbo kadhaa wa kadhaa zikimsifia Mama bila kujali kwamba pembeni ya Mama yupo Baba ndipo niliponyanyua kalamu na karatasi na kuanza kuandika mashairi yanayo msifu Baba, ndivyo alivyoanza kuzungumza Malkia wa bendi ya Supershine Modern Taarab Salma Mbwana.
Queen Salma akiwa na Ally Mikidadi

             Mtandao huu wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com uliamua kumtafuta Queen Salma ili kupata undani zaidi ni nini kilimpelekea kutunga mashairi ya kumsifu Baba wakati bendi nyingi zimekuwa zikimsifia Mama pekee!, Aliendelea kusema kwamba niliona kama thamani ya Baba inapotea bila sababu za msingi, nashukuru mungu kwani wimbo unafanya vizuri sana katika vituo vya redio na hata televisheni, katika wimbo huo Queen Salma amemshirikisha Ally Mikidadi ukipenda muite "High right" wakiimba kwa pamoja.

            Baada ya Queen Salma kufungua milango ya utunzi wa kumsifia Baba sasa bendi zingine nazo wameanza kuamka na kujua kuwa kumbe yupo Baba nae ana umuhimu wake, kwa kulitambua hilo bendi yako ya G5 Modern Taarab wametunga wimbo uitwao Jasho la Baba ambao utaimbwa na kurekodiwa na mwinjuma Muumin ukipenda muite kocha wa dunia. Haya ndio mageuzi yanayotakiwa katika muziki wetu huu wa taarab nchini Tanzania ili tusonge mbele.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni