TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 7 Novemba 2014

AMIN SALMIN:- SINA UGOMVI WALA TATIZO LOLOTE NA MZEE YUSUPH ILA...................

NA KAIS MUSSA KAIS

          Mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com umekuwa ni gumzo mjini kwa kipindi kichache sana tokea kuanzishwa kwake na hii inatokana na utendaji mzuri wa watendaji wake khali iliyopelekea wasomaji kuomba kujua vitu vingi sana vinavyowahusu wasanii na wamiliki wa bendi mbalimbali ni nini wanafanya katika kuufikisha mbele zaidi muziki huu.
MKURUGENZI WA T MOTTO MODERN TAARAB AMIN SALMIN

        Siku tatu zilizopita wakati tupo mitamboni kuwaletea habari tulipata ugeni toka kwa msomaji wetu aitwae Abdul Hemed wa kijitonyama jijini Dar, ambae yeye alijitambulisha kwamba ni mpenzi wa muziki wa Taarab lakini anataka kujua toka kwetu ni nini chanzo cha uhasama na ugomvi wa mkurugenzi wa T MOTTO Amin Salmin, na mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuph

      Sisi kama ilivyo ada yetu tulimuahidi kumpatia majibu rasmi baada ya siku tatu na ni baada ya kufanya mawasiliano na wahusika walizungumzie hili. Leo tulianza na mahojiano na Amin Salmin ambae yeye baada ya kumuuliza hivyo alisema kwakweli sina matatizo na Mzee Yusuph na kama ilitokea ile ya Dar Live kipindi kile ni bahati mbaya tu mambo ya ibilisi, lakini kwa kipindi hiki tupo vizuri tu.

AMIN SALMIN NA MZEE YUSUPH, NYUMA YAO KUNA PICHA NDOGO YA JOKHA KASIM.
        Isipokuwa changamoto iliyokuwepo kati ya mimi na Mzee kwa sasa ni katika muziki tu na wala si vinginevyo, najua na naheshimu uwezo wa Jahazi katika muziki huu wa Taarabu nchini na pia naamini Mzee anakubali uwezo wa T MOTTO katika muziki huu wa Taarabu. Unajua watu wanaongea sana juu yetu, ila ukweli ndio huo, laiti tungekuwa hatupatani basi hata watoto wetu wasingekuwa wanatembeleana na kukaa upande mwingine zaidi ya wiki tatu! hii inaonyesha kwamba kuna maelewano baina yetu.

        Alipotafutwa Mzee Yusuph kwa njia ya simu hakupatikana hewani, kikubwa tunapenda kuchukuwa nafasi hii kuueleza umma wa wapenda Taarabu kwamba wasisikie maneno ya mitaani juu ya hawa watu wapo sawa isipokuwa upinzani uliopo ni katika muziki tu hakuna kingine Wakati huo huo bendi yako ya T MOTTO inatarajia kuachia nyimbo zake mpya mwanzoni mwa mwaka 2015 ili iwe zawadi kwa watanzania wote katika kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya.

.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni