TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 7 Novemba 2014

MWINJUMA MUUMIN:- WABAYA WANGU WANAUMIA, MIMI KUIMBA TAARAB...WATAOMBA POO!.

NA KAIS MUSSA KAIS

               Anaitwa Prince Mwinjuma Muumin, itakuwa vyema zaidi kama utamuita kocha wa dunia vile vile!. Wakati unaachiwa wimbo wa Tunda Dar ilizizima kwa wadau wote wa dansi kila mmoja kwa nafasi yake akikubali uwezo wa kijana huyu, hakuna asiejua uwezo wa muumin katika uimbaji. Muumin anauwezo mkubwa sana wa kuichezea sauti yake atakavyo, anazingatia yale masharti yote ya uimbaji ili asiharibikiwe na uwezo wake kubaki pale pale au kuongezeka zaidi.

MUUMIN AKIIMBA KIGODORO KIMELOWA MAJI "LIVE" NA SAKINA LYOKA WA CLOUDS TV.
          Kwa mara ya kwanza alipoimba wimbo wa Kigodoro kimelowa maji akiwa na bendi ya G5 Modern Taarab wapenzi na mashabiki wa muziki huu walikubali uwezo wake, na sasa anakuja na wimbo mwingine uitwao Jasho la Baba, tena akiwa na bendi ile ile ya G5 Modern Taarab chini ya mkurugenzi Hamisi Slim. siku ya jana nilipata bahati ya kufanya mahojiano nae pale CLUB ESCAPE ONE mikocheni jijini Dar, Na nilipenda kujua haswa msimamo wake katika muziki huu wa Taarab ukoje? ataendelea kurekodi hivi hivi au ana mipango ya kujikita zaidi katika muziki huu nikiwa na maana kufungua bendi yake ya Taarabu?..

HAPA MAHOJIANO YAKIENDELEA NDANI YA ESCAPE ONE MIKOCHENI DAR.
            Mimi ni mwanamuziki ambae mara nyingi huwa nasoma soko linataka nini kwa muda huo, nimekaa nakugundua kwamba soko la muziki huu wa taarab linahitaji mtu kama mimi kuingia huku, ila kuingia kwenyewe ni lazima kuwe kwa hatua na sio kujikita zaidi, nitaendelea kurekodi muziki wa taarab kwani nimependa sana the way nilivyopokelewa, lakini pia sitoacha kupiga dansi, nitaendelea pia kwani wapenzi wa dansi nao bado wanahitaji huduma yangu.

        Mwezi wa kwanza mwakani panapo uhai bendi yangu nitairudisha hapa Dar rasmi na shughuli za kuandaa nyimbo mpya kabisa za Taarab zitaanza, nimeshachagua uongozi wa bendi yangu tayari, na meneja wa bendi hii ni mtu maarufu sana ambae anajulikana sana kwa wapenzi wa Taarab nchini ila sitomtaja kwa sasa ni mapema mno. Kikubwa nawaambia wale maadui zangu wajiandae kuficha sura zao kwani nakuja tena kwa mara ingine.



MWINJUMA MUUMIN KUSHOTO, SAKINA LYOKA KATIKATI NA BI MWANAHAWA ALLY KULIA, WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA.
        Mwinjuma Muumin katika siku kadhaa zijazo anatarajia kwenda studio kurekodi wimbo wa Jasho la Baba akiwa na G5 Modern Taarab, ambao utakuwa ni moto wa kuotea mbali kwani mwenyewe huwa ana sema mara zote huwa habahatishi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni