Bi Mwanahawa Ally au Almaarufu jembe gumu ni muimbaji wa taarabu wa siku nyingi sana hapa nchini tanzania, historia ya safari kimuziki ya Mama yetu huyu imeanzia pale visiwani zanzibar katika bendi ya Culture music enzi hizo, anasema kwamba hii ndio bendi yake ya kwanza kubwa kuifanyia kazi, lakini kabla ya hapo alikuwa akiimba na vikundi vidogovidogo vya mitaani tu huko zanzibar.
SAKINA LYOKA WA CLOUDS TV AKIENDELEA KUFANYA MAHOJIANO NA BI MWANAHAWA ALLY. |
Ndipo nilipoanza kumuuliza Bi mkubwa huyu maswali ya kizushi kama ilivyo ada ya ubuyu wa taarabu, Eti Bi Mwanahawa nasikia umekuwa na tabia ya kuingia mikataba na wenye mabendi alafu mwisho wa siku unakuwa humalizi mkataba huo na kuelekea bendi ingine je kuna ukweli wowote juu ya hilo?.Unajua ndugu Mwandishi waswahili wanasema kwamba "siku zote kitanda usichokilalia huwezi kujua kunguni wake", mimi ni mtu mzima na sasa nina wajuu na vitukuu! kamwe siwezi kufanya upuuzi kama huo nikajishushia heshima yangu, kilichopo hapo ni hawa wenye mabendi kutotimiza masharti ya mkataba tunaowekeana, wanataka waniburuze wanavyotaka wao lakini kunitimizia mahitaji yangu inakuwa mtihani, kamwe siwezi kukaa sehemu kama hiyo.
BI MWAHAWA ALLY AKISISITIZA JAMBO MBELE YA KIPAZA SAUTI CHA CLOUDS TV NA SAKINA LYOKA MAMAA WA DAWA YAO!. |
Bi mwanahawa Ally nilifanya mahojiano nae pale ESCAPE ONE mikocheni siku ya jana baada tu ya kutoka kufanya interview na Bibie Sakina Lyoka wa Clouds Tv mamaa wa dawa yao. kwa sasa Bi Mwanahawa Ally ni msanii wa East African Melody ila pia huwa anapatikana pale G5 Modern Taarab kwakuwa amerekodi zaidi ya nyimbo 2 kwahiyo anaenda kuwapa sapoti vijana wake. Huyo ndio Jembe Gumu linalima mpaka lami.
asante sana UBUYU wa taarab kwa kumhoji Bi Mwanahawa Ally sisi mashabiki tumejua ukweli sasa yupo bendi ya Melody.
JibuFuta