Bendi ya G5 Modern Taarab A.K.A. "Wenyeji wa mji huu", siku ya tarehe 14/11/2014 wanatarajia kutambulisha nyimbo zao mpya kabisa sambamba na wasanii wapya ambao wamejiunga kutoka katika bendi mbalimbali za hapa jijini, katika onyesho hilo ambalo litakuwa na zawadi kwa wapenzi hamsini watakao ingia kwanza kwanza, litasheheni wasanii nguli kabisa wakiwemo mwinjuma muumin na Abdul misambano.
KUNDI ZIMA LA G5 MODERN TAARAB |
Siku ya tarehe 21/11/2014 bendi hiyo itafanya makamuzi yake katika ukumbi wa Eagle Nest Bagamoyo. Pia siku hiyo Bagamoyo zitaimbwa nyimbo mpya kabisa zikiwemo zingine ambazo bado hazijarekodiwa ili kuwapa kitu roho inapenda wakazi wa Bagamoyo na vitongoji vyake. Prince Mwinjuma Muumin na Abdul Misambano wameahidi kufanya mambo makubwa sana siku hiyo hivyo wamewaomba wapenzi na mashabiki kuja kwa wingi kwani hawatojutia kiingilio chao. Kumbuka kuwa show zote hizo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu tano tu kwa kila kumbi!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni