TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 6 Novemba 2014

SAFARI YA ALLY MIKIDADI AU "HIGH RIGHT" KATIKA TAARABU, JE ALITOKEA WAPI?.

NA KAIS MUSSA KAIS

            Muziki wa taarabu nchini umekuwa ukiendelea kujipatia umaarufu kila kukicha na kufanya kuwa ni ajira kubwa ya kudumu na kupelekea watu kuendesha familia zao kupitia fani hii. Taarabu ni muziki wenye asili ya ukanda wa pwani lakini kwa sasa umekuwa ni muziki wa pande zote na umekuwa ukijipatia umaarufu sana.

ALLY MIKIDADI NDANI YA DAR LIVE.
               Ally mikidadi ni muimbaji wa bendi ya Supershine Modern Taarabu ya jijini Dar, lakini hapo kabla alikuwa visiwani zanzibar na vikundi vya taarabu kadhaa wa kadhaa kabla hajapanda boti na kuja jijini Dar kuendeleza fani yake ya uimbaji wa muziki huu. Alipokuwa zanzibar Ally Mikidadi aliimbia vikundi vya Spice Modern Taarab na Sanaa Modern Taarab.

ALLY MIKIDADI AKIWA NA QUEEN SALMA.
          Lakini wakati yupo pale Spice Modern Taarab alifanikiwa kurekodi nyimbo mbili ambazo ni Mtoto ana meremeta Remix, na Wema wangu mtihani, hiyo ilikuwa ni mwaka 2008. Ilopofika mwaka 2009 Ally Mikidadi alikuja jijini Dar na moja kwa moja akajiunga na bendi ya Supershine Modern Taarab ambayo hapo mpaka sasa.

          Supershine Modern Taarab tokea ameingia amesharekodi nyimbo tatu ambazo ni Wambea semeni, Nimempata waukweli na Usia wa Baba ambayo ameiimba akishirikiana na Queen Salma. Huyo ndio Ally Mikidadi ukipenda muite High Right wa bendi ya Supershine Modern Taarab watoto wa magomeni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni