Bendi yako uipendayo ya G5 Modern Taarab, jana ilifanya onyesho lake katika ukumbi wa Flamingo Night Club magomeni mwembechai kama ilivyo kawaida yao kwa siku za jumamosi, wasanii wa bendi mbalimbali nao walikuwepo kushuhudia onyesho hilo kwani G5 imejizolea sifa kubwa za kujaza watu hususani kwa show wanazofanya wao katika ukumbi huo tofauti na bendi zingine.
JUMANNE ULAYA AKIWA KAZINI. |
Mashabiki waliohudhulia onyesho hilo walishangaa wasijue tatizo lipo wapi, badala yake Ramadhan Kisolo aliupiga wimbo ule mpaka ukamalizika, Sisi kama ubuyuwataarabutz.blogspot.com tulimtafuta Jumanne Ulaya aelezee nini sababu iliyomfanya ashindwe kushirikiana na wenzie japo kwa wimbo mmoja tu?.
JUMANNE ULAYA "HAPA KAZI TU". |
Mtandao huu ulimpigia simu mkurugenzi wa G5 Hamisi Slim ili azungumzie hili nae alifunguka kwa kusema, kuna watu wanataka kiki kupitia bendi yetu ya G5, Lakini nawaambia wamechelewa, sisi tunajitambua, tumetulia hatutaki shari wala hasama na mtu!. Sina muda wa kumzungumzia huyo umsemae.
Ubuyuwataarabutz.blogspot.com Tunamuasa Jumanne Ulaya kupunguza ghazabu na kushirikiana na wenzie kwani sanaa ina wigo mpana sana, asahau yaliyopita na kufanya kazi. siku zote hakuna kitu bora katika maisha kama ushirikiano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni