TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 30 Novemba 2014

AMIGO:- SINA MPANGO WA KUIHAMA JAHAZI MODERN TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS

                 Mwezi mmoja uliopita habari zilizokuwa zimezagaa jijini ni kuhusu kusimamishwa kwa AMIGO ndani ya bendi ya Jahazi Modern Taarab kwa utovu wa nidhamu,Lakini ukipata bahati ya kukutana na BABA MAN  mwenyewe hatosita kukuambia kwamba ni kweli alikosea kwa bahati mbaya lakini very soon kila kitu kitaisha na yeye kurudishwa kazini kama kawa kama dawa.

AMIGO MSANII WA JAHAZI MODERN TAARAB
   Kusimamishwa kwa Amigo ndani ya Jahazi Modern Taarab imekuwa kama ni furaha kwa wamiliki wengine wa bendi zingine kwani wamekuwa hawaishi kumshawishi msaani huyu kujiunga nao, eti wakisingizia mzee yusuph alikuwa hamthamini, jambo ambalo sio kweli, Siku zote binadamu huwa wanapenda kuona mwenzao akiharibikiwa, muda huu ilikuwa ni wakati wa kumshauri vyema kijana huyu na sio wafanyavyo wao!.

AMIGO AKIFANYA MAHOJIANO.
        Nilipokutana na Amigo tukazungumza niligundua kwamba Amigo ni msanii anaejitambua, hayupo tayari kukurupuka kwa ushawishi unaoendelea kufanywa na hawa wenye mabendi, Unajua ndugu mwandishi, mimi ni msanii ambae nimekuwa nikifanya mambo yangu kwa malengo, nakubali kosa niliwakosea viongozi wangu lakini kwa sasa tupo sawa na hivi karibuni nitarudi kazini pale pale Jahazi, sina mpango wa kuhamia bendi yoyote ile hata huko Wakaliwao ninapokwenda ni kwa kuwapa kampani tu kama wasanii wengine wanavyofanya naomba nieleweke. Pale Jahazi sijafukuzwa ila nimesimamishwa tu naomba uwaambie wapenzi wangu wanaonimiss. Nitarudi tena katika steji ya Jahazi Very Soon nawapenda sana.

        Mtandao huu unapenda kwanza kumpongeza AMIGO kwa utulivu wake aliouonyesha kipindi chote cha adhabu yake, yamesemwa mengi lakini aliendelea kuwa kimya kupita kiasi, huo ndio ukomavu katika sanaa mungu akubaliki sana AMIGO

.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni