TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 29 Novemba 2014

BI MWANAHAWA ALLY, OMARY KISILA NA ASHURA MACHUPA WAITOSA G5 MODERN TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS

              Siku ya jana ijumaa tarehe 28/11/2014 ilikuwa ni siku ya burudani kwa sehemu nyingi sana hapa nchini hususani ukizingatia week-end ndio ilikuwa imeanza, kwa hapa dar bendi yako ya G5 Modern Taarab ilikuwa inafanya yao ndani ya ukumbi wa CC CLUB msasani.

BI MWANAHAWA ALLY AKIWAJIBIKA STEJI.
          Lakini katika khali ya sintofahamu wasanii wake watatu tena wakutegemewa Bi Mwanahawa Ally, Ashura Machupa na Omary Kisila hawakuwepo katika show hiyo isipokuwa wao walikuwa Dodoma katika ukumbi wa kilimani wakitumbuiza wakazi wa huko. Hii ilipelekea wapenzi wa bendi ya G5 Modern Taarab kuanza kuhoji kulikoni mpaka yatokee haya?.

HAMISI SLIM MKURUGENZI WA G5 MODERN TAARAB.
         Mwashamba Pazi yeye ni mpenzi mkubwa wa bendi hiyo na anaishi kawe jijini Dar, alikuja na familia yake ili waweze kumuona Bi Mwanahawa Ally na Ashura Machupa "LIVE" lakini cha kustaajabisha hawakuwepo watu hao, alilalama na kusema ni bora basi watu hao wasiwe wanawaweka katika yale matangazo yao  wanayobandika mabarabarani, huu ni utapeli, sijafurahi kwakweli alimaliza kwa kusema.

         Bendi yako hiyo ya G5 Modern Taarab leo siku ya jumamosi inatarajia kufanya onyesho lake ndani ya ukumbi wa Flamingo Night Club uliopo magomeni jijini Dar, na kwa vyovyote vile wasanii hao hawatokuwepo kwani inasemekana wanafanya show singida jumamosi ya leo pia.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni