TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 27 Novemba 2014

HATIMAE JAHAZI MODERN TAARAB. KUSHIRIKI MITIKISIKO YA PWANI MWAKA HUU!.

NA KAIS MUSSA KAIS

           Baada ya mtandao huu makini kuripoti vilio vya wadau juu ya kutoshiriki kwa Jahazi Modern Taarab katika Tamasha la mitikisiko ya pwani mwaka huu, uongozi wa redio times na Jahazi wenyewe wamesikia kilio hicho na kutafakali kwa pamoja na kuanzia juzi mtangazaji wa mitikisiko ya pwani times fm khadija shaibu au Didda amekuwa akitangaza kurejea kwa jahazi kwenye tamasha hilo kama ilivyo ada.

KHADIJA SHAIBU- "DIDDA" MTANGAZAJI WA KIPINDI CHA MITIKISIKO YA PWANI TIMES FM 100.5.
       Mdau Mama Najma aliamua kurudi tena ofisini kwetu kuja kutoa shukrani zake kwa mtandao huu kwani anadai bila sisi ubuyuwataarabu.blogspot.com kuripoti habari ile, Bado Jahazi na redio times wangeendelea kushindana bila kufikia muafaka.

KHADIJA YUSUPH- JAHAZI MODERN TAARAB!
     Sisi kwa pamoja kama wadau tunaipongeza Jahazi na redio times fm kwa kuweza kufikia muafaka na kuirejesha tena Jahazi katika tamasha hilo mwaka huu. Mungu ibariki times fm, mungu ibariki Jahazi Modern Taarab!.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni