TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 26 Novemba 2014

KATIKA KUELEKEA MITIKISIKO YA PWANI, RAMADHAN KISOLO KUIHAMA DAR MODERN TAARABU?.

NA KAIS MUSSA KAIS

                  Ubuyu wa Taarabu ni mtandao makini ambao umekuwa ukiibua habari mbalimbali za wasanii wa Taarab zilizo chini ya kapeti na kuziweka hadharani, Kisolo Mwanamalui ni mpigaji gitaa la solo katika bendi ya Dar Modern Taarab, lakini katika siku tatu zilizopita amekuwa akifanya mazungumzo kinyemela na bendi mbili tofauti ili aweze kujiunga na moja wapo.

RAMADHAN KISOLO AKIWA KAZINI.
           Mwandishi wa habari hizi alipopata  udaku huo haraka sana alipiga simu ya Kisolo mwenyewe ili kueleza ni nini ukweli wa jambo hili?, nae alianza kwa kusema, Muziki ndio kila kitu kwangu maisha yangu yote, naendesha familia yangu kwa gharama kubwa sana lakini source ni muziki, kwa sasa nina tatizo linalotaka pesa haraka sana.

RAMADHAN KISOLO.
         Hivyo kuna bendi miongoni mwa bendi hizo mbili inaonyesha nia ya dhati kabisa kunikamilishia matakwa na maslai wangu ili nijiunge nao kikazi, huo ndio ukweli uliopo.Naipenda sana Dar Modern na hata kama nitaondoka kweli basi ni lazima nitaaga wasanii wenzangu pamoja na viongozi pia, alimaliza kwa kusema

        Alipoulizwa mkurugenzi mmoja wapo wa moja ya bendi hizo alisema haoni sababu   ya kumkosa kumchukuwa kisolo mwana malui kwa ni mpigaji mzuri na amenithibitishia kwamba hana mkataba!,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni