TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 26 Novemba 2014

BI MWANAHAWA ALLY NA ABDUL MALICK KUONYESHANA UBABE NDANI YA VILLA PARK MWANZA KESHO!

NA KAIS MUSSA KAIS

              Ukumbi wa Villa Park Mwanza, siku ya kesho
 alhamisi tarehe 27/11/2014 unatarajia kurindima kwa burudani za taarabu za kukata na shoka toka kwa Bi Mwanahawa Ally "Jembe Gumu" sambamba na Abdul Malick toka Mashauzi Classic, show ambayo imeandaliwa na Devota Sotelle mtangazaji wa kituo cha redio cha Passion Fm, kupitia kipindi chake cha Ambaa na Mwambao huko huko mwanza.

BI MWANAHAWA ALLY "JEMBE GUMU".
         Akizungumza na mtandao makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Mtangazaji huyo alisema kwamba ameandaa show hiyo maalum ili kufahamiana na wasikilizaji wake maana amekuwa akisoma sms zao tu redioni pasipo kuwafahamu hivyo basi kupitia show hiyo watajuana na kubadilishana mawazo pia ya kimaisha.

ABDUL MALICK WA MASHAUZI CLASSIC.
         Show hii itakuwa na kiingilio kidogo sana cha shilingi elfu tano "5000/=" kwa mtu mmoja, nimeamua kuweka kiingilio kidogo ili kila mtu aweze kumudu gharama na kuja kupata burudani hii alisema!, Kwa upande wake Bi Mwanahawa Ally aliwaomba wakazi mwanza na mikoa ya jirani kuja kwa wingi kwani amewaandalia burudani ya nguvu na kamwe hawatojutia kiingilio chao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni