TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 26 Novemba 2014

MUSSA MIPANGO ARUDI JAHAZI MODERN TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS

                Yule mpiga gitaa la Bess wa kutegemewa wa bendi ya Jahazi Modern Taarab Mussa Mipango, ambae alikuwa pembeni kidogo na bendi hiyo kwa sasa amerejea rasmi na kuendelea na kazi kama ilivyo kawaida yake.

MUSSA MIPANGO AKIWAJIBIKA.
             Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu Mussa alibainisha kwamba kulikuwa na mambo madogo madogo ambayo alikuwa hajakamilishiwa na uongozi ndipo alipoamua kujiweka pembeni kwanza, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa ndio maana amerudi kazini na anapiga mzigo kama ada.

         Wakati Mussa Mipango alipokuwa ameamua kujiweka kando na bendi ya Jahazi kuna bendi kadhaa zilikuwa zikimnyemelea ikiwemo Ogopa Kopa na G5 Modern Taarab lakini zote zimegonga ukuta na yeye kuamua kurudi katika bendi yake ya awali, Tokea Mussa Amerudi tena kazini, hii inakwenda wiki ya pili.

       Mtandao huu unapenda kumpongeza Mussa Mipango kwa uamuzi wake wa busara aliouamua kwa yeye kukubali kubakia katika bendi ya Jahazi kwani kuhamahama kwa msanii huwa kunafanya wapenzi na wadau wake kukosa muelekeo ni wapi wamfuate.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni