Mkurugenzi wa Tanzania Motto Modern Taarab "T MOTTO" Amin Salmin ametoa tathimini ya mwenendo mzima wa jinsi gani muziki wetu wa taarabu unapo elekea na wapi umetoka, Aliyazungumza haya baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari hizi, Kwamba je nini tathimini yake katika muziki wetu huu wa taarabu kwa miaka hii ya sasa?.
MKURUGENZI WA T MOTTO, AMIN SALMIN. |
Ndugu mwandishi fikilia nyimbo za akina Bi Shakira, Mohamedy Elias, Makame Faki, Juma Balo na wengineo wengi zikipigwa hata leo bado watu wanacheza na kufurahi, ile ndio Taarabu sio haya madebe wanayotengeneza hivi sasa, wimbo haudumu katika redio hata miezi sita! hii ni aibu kwetu sisi tunaojiita mihimili ya muziki huu hapa nchini Tanzania, watangazaji nao wamekuwa na utashi na mapenzi na bendi fulani kitu kinachopelekea hata nyimbo za benndi zingine kukosa nafasi ya kuchezwa hewani, hii sio sawa kiukweli.
Sisi kama mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Tunaomba wadau kutofumbia macho haya yaliyoelezwa na Amin kwani kwa namna moja ama ingine imekuwa ni kero au tatizo kwa mabendi na madirector wengi hapa nchini mwetu, big up! Amin Salmin kwa kufunguka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni