TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 24 Novemba 2014

WADAU WALALAMA, KWA JAHAZI KUJITOA MITIKISIKO YA PWANI MWAKA HUU!.

NA KAIS MUSSA KAIS

            Kitendo kilichofanywa na bendi ya Jahazi Modern Taarab, kujitoa katika hatua za mwisho kwenye tamasha kubwa la Taarab nchini Tanzania la Mitikisiko ya Pwani linaloandaliwa na kituo cha redio cha Times Fm 100.5 cha jijini Dar kimelalamikiwa na wapenzi pamoja na wadau wao na kuwaomba uongozi wa Jahazi na Times Fm kukaa mezani tena na kupata muafaka ili na wao waweze kupata burudani ya bendi hiyo siku ya tamasha.

MZEE YUSUPH.
        Akizungumza na mtandao huu ofisini kwetu mwananyamala mshabiki mmoja aliejitambulisha kama Mama Najma amesema amesikitishwa sana na taarifa hizi kwani yeye ni mpenzi mkubwa wa bendi ya Jahazi na kila inapopiga amekuwa akihudhulia maonesho yao.Amemuomba Mzee Yusuph kukaa tena na redio Times ili wafikie muafaka wa tatizo hili, na kama itashindikana basi yeye hatokwenda katika tamasha hilo mwaka huu.

FATMA NYORO.
        Mtandao huu ulimpigia simu kiongozi wa bendi ya Jahazi Modern Taarab Hamisi Boha na kutaka ufafanuzi juu ya jambo hili nae alizungumza kama ifuatavyo. Sisi Jahazi hatujakataa kushiriki katika tamasha la mitikisiko ya pwani mwaka huu ila ratiba ya show zetu imebana sana, tuna show mpaka mwezi wa kwanza, nikiwa na maana huu mwezi wa kumi na mbili wote bendi imekodiwa na wameshalipa pesa zao tayari wanasubili sisi Jahazi kutekeleze tu, sasa hapo tunafanyaje ndugu mwandishi alihoji?.

           Sisi tunakiheshimu sana kituo cha redio cha times fm na tamasha la mitikisiko ya pwani kwa ujumla ila tunaomba watuelewe pamoja na wapenzi wetu pia tunawapenda sana. Baada ya Jahazi kutowa taarifa kwamba hawatoshiriki, inasemekana kituo cha times fm wameamua kumuongeza Msagasumu kabali yao au ukipenda muite mzee wa radha. Bendi zitakazo shiriki mwaka huu ni

           1. Wakaliwao Modern Taradance
           2. Mashauzi Classic Modern Taradance
           3. East African Melody
           4. Dar Modern Taarab
           5. Khadija Kopa na Ogopa Kopa
           6. Msagasumu kabali yao au mzee wa radha na kisingeli!.

MZEE YUSUPH NA KHADIJA YUSUPH.
         Sisi mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com tunaitakia redio times fm maandalizi mema ya tamasha hilo kwani kila mwaka limekuwa likifanya vizuri sana hivyo hata mwaka huu litatia fora kwa ubora wake.


Maoni 1 :